MAKALA BIASHARA HARAMU YA BINADAMU:
BIASHARA HARAMU YA BINADAMU
Nianze kwa kukupa tafsiri kwa ufupi, au maana ya Biashara haramu ya Binadamu au kama wengine wakitambua kama, Usafirishaji haramu wa binadamu nami niseme yote sawa, hii Ni biashara ya binadamu kwa madhumuni ya kazi ya kulazimishwa, utumwa wa ngono, kutumikishwa katika kazi hata kuchukuliwa viungo vya mwanadamu na kuuzwa kwa bei ghali.
Usafirishaji haramu wa binadamu ni biashara inayogusa mtu, hasa wanawake na watoto, na haihusishi harakati za mtu kutoka sehemu moja hadi nyingine, na unaweza kutokea ndani ya nchi au nje ya nchi.
Namini kwa tafsiri hiyo fupi umepata mwanga sasa wa kile nimekusudia kukupatia japo kwa uchache kuhusu biashara haramu ya binadamu.
Takwimu zinaonesha kwamba, hadi sasa kuna zaidi ya watu milioni 45 ambao wametumbukizwa katika biashara hii inayozalisha kiasi cha dola za kimarekani bilioni 32 sawa na Bilioni 74,784 kwa mwaka, na hivyo, kuchuana kwa karibu sana na biashara haramu ya silaha na dawa za kulevya duniani.
Wanawake, wasichana na watoto wadogo ndio walengwa wakuu wa mifumo hii ya utumwa lakini hata wanaume pia nao ni waathirika japo kitakwimu si sawa na hilo kundi la awali.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa zinasema kuna ongezeko la asilimia 58 la usafirishaji wa watu duniani, swali langu je, nini kifanyike ili kukabiliana na suala hili? Hawa ni baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma wana maoni katika hili.
Je, Serikali nchini imefanya jitihada gani za kuzuia biashara haramu ya usafirishaji binadamu? Na je nini wamekibaini kama kiini cha biashara hiyo? Bw. Datus Magere ni Mwenyekiti Tume ya kuzuia Biashara haramu nchini.
Kwa mujibu wa ripoti ya ubalozi wa Marekani nchini kwenye maadhimisho ya kupinga biashara ya usafirishaji binadamu ya mwaka 2019 katika ukurasa was aba wa ripoti hiyo yenye kursa kumi na moja, kipengele cha kuzuia ripoti inasomeka kuwa, Serikali ya Tanzania ilitenga bajeti ya milioni 100.5 za Tanzania ($43,790) kwa ATS, kitengo cha ngazi ya chini cha kuzuia biashara haramu ya usafirishaji binadamu, kiwango sawa kama cha mwaka uliopita.
Kamati ya kuzuia biashara haramu ya usafirishaji binadamu, inayosimamia utendaji na mwelekeo wa ATS, walikutana mara mbili wakati wa kipindi cha ripoti hiyo, Serikali ilipitisha mpango kazi mpya wa kitaifa, kuanzia mwaka 2018-2021; hata hivyo, jitihada za kutekeleza mpango mpya au kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wake ulikuwa wa kiwango cha chini katika kipindi chote cha ripoti.
Kutokana na uhaba wa fedha, ATS haikufanya kampeni yeyote kuhamasisha umma kuhusu biashara haramu ya usafirishaji binadamu wakati wa kipindi cha ripoti.
Unaweza dhani tatizo lipo katika taifa letu pekee bali ni janga la kimataifa, nchini Kenya hali ipoje, huyu hapa Wini Mtevu kutoka Taasisi ya Heart Kenya inayojishughulisha na uzuiaji wa biashara haramu ya bianadamu anaeleza…
Tatizo la usafirishaji na biashara haramu ya binadamu linaongezeka kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa zilizotolewa mwanzoni mwa mwaka huu wa 2019 kote duniani.
Pia takwimu zilizotolewa na shirika la kazi duniani ILO mwishoni mwa mwaka 2018 zinasema watu takribani milioni 40 kote duniani bado ni waathirika wa utumwa au kutumikishwa kinyume cha matakwa yao.
Je, sheria inatamka nini juu ya haki na usawa wa mwanadamu, Gothad Mwingira ni wakili wa kujitegemea kutoka Justice Watch Jijini Dodoma.
Shirika la Kimataifa la Wahamiaji IOM, linafafanua kwamba, biashara haramu ya binadamu inaendelea kushamiri sana duniani kutokana na wimbi kubwa la wahamiaji na wakimbizi, Biashara hii Barani Afrika inakadiriwa kufikia kiasi cha dola za kimarekani milioni 400 kwa mwaka.
Ni fedha inayolipwa kwa wafanyabiashara haramu kwa njia ya gharama za usafiri jangwani na baharini sanjari na kazi za suluba ughaibuni huku waathirika wakitoka nchi za Somalia, Sudan ya Kusini, Eritrea, Mali, Senegal, Gambia, Chad, Niger na Nigeria na wengine ni wale wanaotoka Bangaladesh.
Naamini umejifunza na kutambua kuwa kuna ukatili mwingine wa uliokidhiri na ambao umekuwa mfupa mgumu kwa mataifa yote ulimwenguni nao ni Biashara haramu ya Binadamu, kwa Pamoja tuungane kukemea na kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi wa vitendo hivi ili kuwa na jamii iliyo salama kwa Maisha bora na kufika Pamoja kwenye malengo ya milenia ya umoja wa mataifa 2030.
Imeandaliwa na: Samwel Vickness Andrew (Baba Chibwetele)