Takriban watu 22 waliuawa baada ya vitambulisho kukaguliwa nchini Pakistan

0

Watu wenye silaha wamewaua takriban watu 22 kusini-magharibi mwa Pakistan baada ya kuwalazimisha kutoka kwenye magari yao na kuangalia utambulisho wao, maafisa wanasema.

Shambulio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo kwenye barabara kuu ya mkoa wa Balochistan, ambapo vikosi vya usalama vinapambana na ghasia za kidini, kikabila na kujitenga.

Watu hao waliokuwa na silaha walikagua hati za utambulisho, wakiripotiwa kuwatenga wale kutoka Punjab ili wapigwe risasi, kabla ya kuwasha moto magari, maafisa walidai.

Kundi la wapiganaji wa Baloch Liberation Army (BLA), limesema ndilo lililohusika na mashambulizi katika wilaya ya Musa Khel.

Katika muda wa saa 24 zilizopita, BLA imeanzisha mfululizo wa mashambulizi kwenye mitambo mingi ya serikali – ikiwa ni pamoja na vituo vya polisi na kambi za vikosi vya usalama katika jimbo lote.

Huko Kalat, 11 waliuawa – watano kati yao wakiwa maafisa wa usalama – na miili sita ilipatikana katika wilaya nyingine huko Balochistan.

Kulingana na Najibullah Kakar, afisa mkuu wa eneo hilo, karibu wanamgambo 30 hadi 40 walihusika katika Musa Khel.

“Walisimamisha magari 22,” aliambia shirika la habari la AFP. “Magari yaliyokuwa yakisafiri kwenda na kurudi Punjab yalikaguliwa, na watu kutoka Punjab walitambuliwa na kupigwa risasi.”

BLA imesema ilikuwa inalenga wanajeshi wanaosafiri wakiwa wamevalia kiraia, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Kabla ya shambulio hilo, BLA ilionya umma wa Baloch kukaa mbali na barabara kuu, na kuongeza kwamba “vita vyao ni dhidi ya jeshi la Pakistani linalokalia”.

“Tumechukua udhibiti kamili wa barabara kuu zote kuu kote Balochistan, na kuzizuia kabisa,” iliongeza.

Waziri Mkuu Shehbaz Sharif alionyesha “huzuni kubwa na kulaaniwa kwa shambulio la kigaidi” katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake.

Balochistan ni jimbo kubwa zaidi la Pakistani lakini, ingawa lina rasilimali nyingi kuliko majimbo mengine, ndilo lenye maendeleo duni.

BLA na wengine wanaotaka kujitenga kwa Baloch wamezidisha mashambulizi dhidi ya Wapunjabi na Wasinhdi kutoka sehemu nyingine nchini Pakistani wanaofanya kazi katika eneo hilo. Pia wamelenga makampuni ya nishati ya kigeni wanayoshutumu kwa kunyonya eneo hilo bila kugawana faida.

Katika tukio sawia la Aprili mwaka huu, abiria tisa walishushwa kutoka kwenye basi moja huko Balochistan na kuuawa kwa kupigwa risasi baada ya vitambulisho vyao kukaguliwa.

Nchi kadhaa za Magharibi, zikiwemo Uingereza na Marekani, zimeteua BLA kama shirika la kigaidi la kimataifa.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x