Dozi Laki 1 ya chanjo ya Mpox leo kupokelewa leo DRC

0

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo Alhamisi Septemba 5 itapokea shehena ya kwanza ya dozi takribani 100,000 za chanjo ya Ugonjwa wa homa ya Mpox.Seŕikali ya Kongo imepanga kuanza zoezi la utoaji wa chanjo ya Mpox mwishoni mwa juma hili.

Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC, kimeongeza kuwa jumla ya chanjo laki 200,000 zitawasili nchini humo kufikia mwishoni mwa wiki hii.

Jumla ya chanjo 200,000, katika makundi mawili, zitasafirishwa kwa ndege hadi Kinshasa kati ya siku ya Alhamisi Septemba 5 na siku ya Ijumaa Septemba 6.

Baadaye chanjo hizo zitasambazwa kati ya Goma, Lubumbashi na mji mkuu wa Kongo. Dozi milioni tatu laki sita zilizopatikana na Africa CDC zitahamishwa, katika siku kumi na tano zifuatazo, hadi nchi nyingine za Afrika (Gabon, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Côte d’Ivoire) zilizoathiriwa na mlipuko wa Mpox, anasema mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC, Jean Kaseya

2.7 3 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x