Cristiano Ronaldo amefikia hatua muhimu Alhamisi kwa kufunga bao la 900 katika maisha yake ya soka
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 aliifungia Ureno katika mchezo wao wa Ligi ya Mataifa dhidi ya Croatia, na kuwaweka mbele kwa mabao 2-0 .
Ilisababisha sherehe ya kihisia kwa fowadi huyo, huku akipiga magoti kando ya bendera ya kona huku akilia.
Bao hilo lilikuwa la 131 kwake kwa nchi yake, huku akiwa amefunga pia katika ngazi ya klabu za Sporting Lisbon, Manchester United, Real Madrid, Juventus na klabu ya sasa ya Al-Nassr.
Kufunga kwa zaidi ya miongo miwili – mabao ya Ronaldo
Huo ndio maisha marefu ya Ronaldo kwamba ikiwa mtu alizaliwa wakati alifunga bao la kwanza la ushindani katika maisha yake ya soka sasa wangekuwa 21.
Alifunga mabao mawili kwa Sporting ya Ureno tarehe 7 Oktoba 2002, akiwa na umri wa miaka 17 miezi minane na siku tatu katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Moreirense.
Kisha akahamia Manchester United, akifunga mabao 118 katika mechi 293 akiwa na Mashetani Wekundu kabla ya kujiunga na Real Madrid mwaka 2009 kwa rekodi ya dunia ya euro 94m (£80m).
Kwa miaka tisa akiwa na wababe hao wa Uhispania alifunga mabao 450 katika mechi 438 pekee kabla ya kwenda Italia kujiunga na Juventus.
Aliongeza mabao mengine 101 kwenye jumla ya mabao yake katika kipindi cha miaka mitatu akiwa na klabu hiyo ya Italia kabla ya kurejea United, ambapo angefunga mabao 27 katika michezo 54.
Lakini kurejea kwa Mashetani Wekundu hakukuwa na mwisho wa hadithi na mnamo 2023 alihamia Saudi Arabia na Al-Nassr ambapo amefunga mabao 68 na kuhesabu.