Takriban wanafunzi 17 wameuawa katika ajali ya moto shuleni Kenya – polisi

0

Takriban wanafunzi 17 wamefariki baada ya shule moja katikati mwa Kenya kushika moto Alhamisi usiku, polisi walisema.

Kuna hofu kuwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka kwani wengine zaidi ya kumi wamepelekwa hospitalini wakiwa na majeraha ya moto.

Chanzo cha moto katika shule ya msingi ya Hillside Endarasha kaunti ya Nyeri bado hakijajulikana.

Rais William Ruto aliutaja moto huo kuwa “wa kutisha” na “wa kuangamiza”, na ameagiza uchunguzi ufanyike.

“Waliohusika watachukuliwa hatua,” Bw Ruto aliandika kwenye mtandao wa kijamii.

Timu ya wachunguzi imetumwa shuleni, polisi walisema.

Msemaji wa polisi Resila Onyango ameliambia shirika la habari la AFP kwamba miili iliyookotwa “ilichomwa kiasi cha kutoweza kutambulika”.

“Miili zaidi ina uwezekano wa kupatikana mara (eneo) litakaposhughulikiwa kikamilifu,” aliongeza.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema linatoa huduma za usaidizi wa kisaikolojia kwa wanafunzi, walimu na familia zilizoathiriwa, na limeanzisha dawati la kufuatilia shuleni.

Moto wa shule ni wa kawaida katika shule za bweni za Kenya.

Mnamo 2017, wanafunzi 10 walikufa katika shambulio la uchomaji moto katika Shule ya Upili ya Moi Girls katika jiji kuu la Nairobi.

Takriban wanafunzi 67 walifariki katika Kaunti ya Machakos, kusini-mashariki mwa Nairobi, katika tukio baya zaidi la uchomaji shule nchini Kenya zaidi ya miaka 20 iliyopita.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x