Kuondolewa kwa Gachagua kuchapishwa kwenye gazeti la serikali, Rais Ruto apanga kumteua DP mpya

0

Spika wa Bunge la Seneti Amason Kingi ametangaza kushtakiwa kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na hivyo kurasimisha kuondolewa afisini kwa kiongozi wa pili nchini.

Notisi ya Gazeti la Oktoba 17, 2024, ilitolewa jana usiku mara baada ya Seneti kuidhinisha hoja ya kumtimua Gachagua.

Katika notisi hiyo, Spika wa Seneti aliorodhesha misingi mitano kati ya 11 ambayo Seneti ilipiga kura kumtaka Gachagua arejeshwe nyumbani.

Sababu tano za kushtakiwa kwa Gachagua zilizoidhinishwa na Seneti ni pamoja na;

1. Ukiukaji mkubwa wa Vifungu 10 (2) (a), (b) na (c); 27 (4), 73 (1) (a) na (2) (b); 75 (1) (c), na 129 (2) ya Katiba na Ibara ya 147 (1), kama inavyosomwa pamoja na Ibara ya 131 (2) (c) na (d) ya Katiba.

2. Ukiukaji mkubwa wa Ibara ya 160 (1) ya Katiba ya Uhuru wa Kitaasisi na Kimaamuzi wa Majaji.

3. Ukiukaji mkubwa wa Ibara ya 3 (1) na 148 (5) (a) ya Katiba kuhusu uaminifu kwa Kiapo cha Ofisi na Utii.

4. Sababu kubwa za kuamini kwamba Mheshimiwa Naibu Rais ametenda uhalifu chini ya vifungu vya 13 (1) (a) na 62 vya Sheria ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa.

5. Utovu mkubwa wa nidhamu ambao haukubaliani na wito wa juu na hadhi ya heshima ya Ofisi ya Naibu Rais na mjumbe wa Baraza la Mawaziri na Baraza la Usalama la Kitaifa. Mheshimiwa Naibu Rais ameshambulia na kuhujumu kazi ya Idara ya Usalama wa Taifa na Maafisa wake.

Kufuatia kuondolewa kwa Gachagua, Rais anatarajiwa kuteua atakayechukua nafasi hiyo na kuwasilisha jina hilo kwa Bunge la Kitaifa ili kuidhinishwa.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x