Serikali yajipanga kudhibiti matukio ya kiuhalifu yanayotokea sehemu mbalimbali nchini na hatua kuchukuliwa

0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amekutana na kufanya kikao na Uongozi wa Jeshi la Polisi nchini ukiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura ambapo kikao hicho kilihusu mambo yanayohusu Usalama na Amani ya nchi ikiwemo kujadili matukio ya kiuhalifu yanayotokea sehemu mbalimbali nchini na hatua zinazochukuliwa kuendelea kudhibiti matukio hayo.

Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma kimehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi ambapo kwa upande wa Jeshi la Polisi kilihudhuriwa na Viongozi wafuatao Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu, Suzan Kaganda, Kamishna wa Fedha na Lojistiki, Liberatus Sabas, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Awadh Juma Haji, Kamishna wa Sayansi ya Uchunguzi wa Jinai, Shabani Hiki, Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi,Ramadhani Kingai, Msemaji wa Jeshi la Polisi,Naibu Kamishna,David Misime, Naibu Kamishna kutoka Kamisheni ya Intelijensia na Jinai,Kheriyangu Khamis Mgeni,Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Jumanne Muliro.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x