“HUENDA KIM JONG UN AMENYONGA VIONGOZI 30”

0

Korea Kusini imesema Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un huenda aliamuru Maafisa wasiopungua 30 wa Serikali kunyongwa baada ya mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya maelfu ya Watu Nchini humo.

Televisheni ya kusini ya Chosun imeripoti jana September 03, 2024 kwamba Mamlaka ya Korea Kaskazini iliwahukumu kati ya Watu 20 hadi 30 adhabu ya kifo mwezi uliopita kwa kushindwa kuzuia athari za mafuriko hayo mabaya.

Ingawa ni vigumu kujua maelezo ya kina kutokana na usiri uliokithiri wa Nchi hiyo, Shirika la Habari Nchini humo (KCNA) limeripoti kwamba Kim aliamuru Mamlaka kuwaadhibu vikali Maafisa hao baada ya mafuriko makubwa katika Mkoa wa Chagang, karibu na mpaka wa China.

Vyombo vya Habari vya Serikali ya Korea Kaskazini viliripoti kuwa mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa mwezi July iliacha zaidi ya nyumba 4,000 pamoja na majengo mengine mengi ya umma, miundo, barabara na reli zimejaa maji katika mji wa kaskazini-magharibi wa Sinuiju na mji jirani wa Uiju.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x