Mbowe ajitokeza Magomeni, akamatwa na Polisi

0

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekamatwa na Polisi eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 23, 2024.

Kabla ya Mbowe kukamatwa, alifika eneo hilo akiwa na gari dogo, kisha kuanza kuzungumza na waandishi wa habari.

Septemba 11, 2024, Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na mauaji, akiwemo kada wake, Ali Kibao. Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku.

Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuweka mkazo suala hilo, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.

Amesema jambo lingine waliloliomba ni kurejeshewa kwa viongozi wa chama hicho, waliotekwa kwa nyakati tofauti wakiwa hai au hali ya umauti, akiwemo Deusdetith Soka, Dioniz Kipanya, Jacob Mlay na Mbwana Kombo.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x