Uganda yaadhimisha miaka 62 tangu ipate uhuru

Wakati Uganda inaadhimisha miaka 62 ya uhuru kutoka kwa wakoloni wa Uingereza yaliyofanyika katika wilaya ya Busia mashariki mwa Uganda, Rais Yoweri Museveni ametoa wito wa uzalishaji mali, na kusisitiza ongezeko la thamani katika mazao ya kilimo.

Rais Museveni amesema kuwa tatizo la Afrika na makoloni mengine ni kuzingatia kuzalisha malighafi pekee, jambo ambalo limekuwa na madhara kwa bara la Afrika, akibainisha kuwa Uganda imeongeza thamani ya bidhaa zake kwa makusudi ili kuingiza mapato zaidi ya mauzo ya nje. Ameongeza kuwa chini ya mipango mbalimbali ya maendeleo ya serikali, takriban asilimia 67 ya wakazi wa Uganda sasa wanashiriki katika uchumi wa fedha.

Rais Faustin-Archange Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya Kati aliyefanya ziara nchini Uganda pia ameshiriki kwenye sherehe hizo, akimpongeza rais Museveni kwa uongozi wake, kwa sababu ameifanya Uganda kuwa nchi nzuri ya maridhiano ya kitaifa.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x