Chelsea wamemsajili Sancho kwa mkopo kutoka Man Utd

Chelsea wamemsajili winga wa Manchester United Jadon Sancho kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Mkataba huo unajumuisha wajibu kwa Chelsea kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 24, kwa kati ya £20-25m msimu ujao wa joto.

Sancho alijiunga na United kwa mkataba wa pauni milioni 73 kutoka klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund Julai 2021 lakini amekuwa na wakati mgumu Old Trafford.

Alicheza mechi 83 katika misimu mitatu kamili lakini alikuwa na ugomvi wa hali ya juu na meneja Erik ten Hag ambayo ilimfanya afanye mazoezi mbali na kikosi cha kwanza.

Baada ya kujiunga tena na Dortmund kwa mkopo mwezi Januari, alirejea United majira ya joto na hajawa kwenye kikosi kwa mechi zao zote za Ligi Kuu hadi sasa.

Mechi ya mwisho kati ya mechi 23 alizocheza England ilirejea mwaka 2021, baada ya kupuuzwa kwa Euro 2024 na Kombe la Dunia huko Qatar mnamo 2022.

‘Njia bora ya kutoka kwa hali mbaya’

Jadon Sancho na Erik ten Hag wakati wa maandalizi ya msimu mpya
Maelezo ya picha,Jadon Sancho alikuwa na Manchester United kwenye ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya

Mtangazaji mkuu wa habari wa soka wa BBC Sport Simon Stone :

Kwa Manchester United, mkataba huu unawakilisha njia bora ya kutoka katika hali mbaya.

Mkurugenzi wa michezo Dan Ashworth, mkurugenzi wa ufundi Jason Wilcox na mtendaji mkuu Omar Berrada wamelazimika kutafuta njia ya kutoka kwenye tatizo kubwa ambalo si la wao.

Sancho tayari alikuwa ametofautiana na Erik ten Hag wakati safu ya watu watatu wakuu ilipowekwa. Usuluhishi uliojadiliwa ili kumrejesha Sancho kwa mazoezi ya kabla ya msimu mpya na kwenye ziara ya klabu hiyo nchini Marekani ulikuwa hali ya muda ambayo ilimruhusu kubaki na utimamu wake, na hivyo kurahisisha kupata klabu mbadala ya kuendelea na soka lake.

Ukweli ni kwamba hata kabla ya kugombana kwake hadharani na meneja wake, Sancho aliahidi mengi zaidi kuliko aliyoitoa kwa klabu hiyo ya Old Trafford.

United wanajaribu kuunda ukweli mpya na kuibuka kwa Alejandro Garnacho msimu uliopita na Amad Diallo mwanzoni mwa msimu huu kumewapa Ten Hag chaguzi nyingine kwa nafasi pana, hata bila kuwajumuisha Marcus Rashford na Antony.

Ni huruma kwa kila mtu hatua hiyo haikufanya kazi. Kwa kuzingatia yote yaliyotokea, suluhisho hili sio kubwa. Lakini ni njia bora ya kutoka.

‘Sancho anakuja kwa bei nzuri’

Mwandishi wa habari wa BBC Sport football Nizaar Kinsella:

Kwa Chelsea, swali la kumsajili Sancho litakuwa tu, kwanini?

Wanao Christopher Nkunku, Nicolas Jackson, Pedro Neto, Mykhailo Mudryk, Noni Madueke, Cole Palmer, Joao Felix na Marc Guiu kwenye safu yao ya ushambuliaji.

Lakini watabishana kwamba Sancho anakuja kwa bei nzuri na kwamba anaweza kufuata mkondo wa Cole Palmer ikiwa ataruhusiwa kurejea kwenye ubora wake.

Kuna wafanyakazi wengi wa zamani wa klabu ya Manchester City katika klabu hiyo, akiwemo meneja Enzo Maresca na mtaalamu mashuhuri wa kuajiri Joe Shields.

Huyu ni mchezaji ambaye, kwa maneno ya Maresca, “anajua” na hatimaye anaweza kuendana na mfumo wake.

Chelsea pia wanapenda kusajili wachezaji waliowasaidia wakiwa watoto, na Sancho aliyezaliwa kusini mwa London anafaa.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x