Raia aliyekamatwa na mafuvu 24 ya vichwa vya binadamu Uganda anakabiliwa na kifungo cha maisha jela

olisi nchini Uganda, inasema raia wake mmoja aliyekamatwa hivi karibuni akiwa na mafuvu 24 ya vichawa vya binadamu, huenda alikuwa anavitumia kwa utoaji kafara na anakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

Aidha amesema katika uchunguzi uliofanyika katika makazi yake, walipata mabaki ya wanyama na ngozi, polisi ikisema inaendelea kupekua eneo lake kwa imani ya kupata mabaki zaidi ya binadamu.

Kwa mujibu wa RFI Godfrey ambaye alidai ni mganga wa jadi na tiba asilia, amekanwa kufahamika na shirikisho la kitaifa la waganga wa jadi na tiba asilia la Uganda

Akinukuliwa na shirika la utangaza la Uingereza msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda, Patrick Onyango, amesema mtuhumiwa Dhamulira Godfrey, atashtakiwa chini ya sheria ya kuzuia na kudhibiti utoaji kafara za binadamu.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x
Scroll to Top